FILAMU YA KOMEDI YA WEMA, KITIME NA MASANJA KUZINDULIWA IJUMAA
-->
FILAMU YA KOMEDI ILIYOKUWA AMBAYO IMETENGENEZWA NA KAMPUNI
MPYA YA WEMA SEPETU(ENDLESS FAME FILMS),
ITAZINDULIWA WIKI HII. FILAMU HIYO AMBAYO SCRIPT IMEANDIKWA
NA MWANAMUZIKI JOHN KITIME, PIA ITAKUWA NA WACHEKESHAJI MAARUFU KAMA MASANJA,
JOTI, BAMBOO,SENGA NA YEYE MWENYEWE KITIME AKICHUKUA NAFASI YA MUME WA WEMA
SEPETU, AMBAYE KATIKA FILAMU HII AMECHUKUA NAFASI YA MKE WA MKURUGENZI WA
KAMPUNI YA KUZOA TAKA. NI FILAMU ILIYOJAA VICHEKESHO VYA KUVUNJA MBAVU. MASANJA
NI DEREVA WA GARI LA TAKA, WAKATI BAMBO NI MWENYEKITI WA MTAA AMBAO UMEPATA
ZAWADI YA MTAA WENYE USAFI BORA, WAKATI JOTI AMECHUKUA NAFASI YA MZEE ALIYESTAAFU WIZARA YA AFYA. WASANII WENGINE
WALIOMO NI MONA LISA, NATASHA, VANITHA NA MWANAMUZIKI WA MSONDO ROMA. UZINDUZI WA FILAMU HII
UNATEGEMEWA KUFANYIKA MLIMANI CITY IJUMAA JIONI