Karibuni.... Welcome.... Karibuni...
Blog hii ni ya wajanja wote wanaopenda mambo mazuri kwenye ulimwengu huu wa kaijanja!!!!
Ingia kila siku kupata mambo mapya kama news, picha, tetesi, matukio yoote ya town n.k....
Ilikuwa siku ya ijumaa nlipokea sms,"hi, hw ru boy? Hv ni wewe unayeonekana kwenye tangazola tiGO? Plz nijibu... Lucy"nkitafakari ni new # lkn hakuna haja ya kumficha, nkachukua maamuzi ya kibinadamu nkamjibu,"hi back, i'm fne, ni mm ndio dadangu..."ilinichukua muda wa 3hrs nkapata tena txt"Je, unaishi dar sehemu gani?"kwakuwa sikuisave ile namba ya Lucy nkajikuta najibu"samahan nani mwenzangu? Napenda kukufahamu kabla sijakuambia nilipo.."akapiga akalalamika..."jaman Erick ujasave my #? Sawa bana ndo zenu mkishakuwa mastaa!"nkamfafanulia,"mbona hii ni mara yangu ya kwanza kuongea na ww? Dadangu nikumbushe samahani bado cjajua ww ni nani mwenzangu?"akaongeza pozi..."kwani hakuna namba iliyokutumia txt leo inafanana na hii?"mmmh nkavuta kumbukumbu txt kama 21 nmezipokea kwa siku hiyo na new # ni kama 6 sasa ni ipi kati ya hizo? Ikabidi nmsihi anikumbushe"hiyo txt ilikuwa imeandikwaje best?"akapata maudhi na kunichana live..."aaah wapi unajidai ukumbuki Erick yaan kitangazo kimoja tu unaleta pozi hivyo kakangu ungekuwa Kanumba je? Yaan huikumbuki hii namba ww?"hapo nilianza kuingiwa na fikra za taarabu..."Samahan dadangu, unaniruhusu kukata simu, au unahita kupata kifurushi cha dharau kutoka kwangu?"hivyo ndivyo uungwana ulivyoniagiza kumjibu..."aaaah kwenda huko kwanza tangazo lenyewe lile aaagh ms*#?!* nn?"akakata simu... Kwakuwa nlikuwa namwandikia script mwana akagonge video ya ngoma yake, alipatwa mshangao sana kuniona nikiiangalia ile simu na sura yangu ikionyesha kuchukizwa na maongezi yaliyokatishwa muda huo..."Ballo vipi tena kuna msiba nn?"aliniuliza mwanangu anaitwa Chriss huwa ananiita Ballo kama a.k.a yangu lkn jina langu siku zote ni Erick..."aaah basi tu kuna dada kaniudhi tu halafu hata simfahamu, na hatak hata kujitambulisha! Aaagh basi tena ndio kashantukana tuendelee na kazi, nikayeyushia na kurudi mzigoni... Siku ile ilipita na maisha yakaenda kama kawaida wala sikuwaza kumpigia yule dada, hata hakuntxt siku inayofata kuna kimeo nilipata maeneo ya Victoria nkatimba na wanangu kama vile bongo ilivyo wakachagua cast zao walizopanga sisi wengine ikawa kama tunasindikiza tu, majina yetu na picha zikakusanya sisi tukawa tupo nje tunasubiri na kubadilishana mawazo akaja mshkaji akapenda kujua..."Ballo kwann unaonekana tofauti sana na lile tangazo? Au yule ni kakayako nn? Mbona kuleni kama umezeeka zaidi ya ulivyo?"wanangu wakanijibia kuwa lile tangazo lilikuwa na lengo la kupata sura za kitanzania so ilibidi editor anitengeze vile kupata kile wanachohitaji.. . Heeh eti aliondoka na baada ya dk4 akarudi na warembo kama wanne nao walikuja kunipongeza kwa kula shavu tukafahamiana kumbe ni models, storry hapa pale hadi muda wa kuitwa majina wakachaguliwa waliochaguliwa sisi tukasepa yule mshkaji akaniomba # nikampa ila sijui kwann nlisahau kuchukua ya kwake! Iyo ilikuwa jumamosi ilipofika j2 nlitoka sinza mori nakoishi nkapanda gari za gongolamboto niende ilala yule mwana alinipigia jana yake usiku na kujitambulisha yeye ni Salimu tuliyeonana kule victoria ananialika kwenye party ya birthday ya moja ya wale warembo walionisalimia na inafanyika suncirt beach so niwahi tuondoke nae... Dar foleni kama kawa lkn ilizidi sana maeneo ya ilala sokoni kuna wakati hadi unatamani kushuka uchukue bodaboda ila nkavumilia tu,"Nkimuona ntamjua tu.. Ilikuwa ndio napeleka kwenye M-Pesa jamani mimi jamaaani...!!!" ilikuwa ni sauti ya mwanamama akilalamika kwa nnje ameibiwa huku watu wakikusanyika kujua kilichojiri, kwakuwa kulikuwa na foleni na mm nlikuwa nimesimama kwa mlangoni mbele ya konda basi nliweza kushuhudia vizuri jinsi yule mama alivyokuwa akilia na kumuonea huruma..."Si huyu hapo jamani ndio yeyee...!"ilikuwa ni sauti ya dada mmoja alikuwa pembeni kidogo na wenzie wawili akininyooshea mm kidole... Watu wote waligeuka na kuniangalia na mm nkibaki kumshangaa yule dada aliyeonekana kunitambua..."Eeh ndio yeye! Onaa eti anashangaa!!!"Baada ya sekunde10 nlikuwa katikati ya mgambo na shati langu likiwa limechanika na puani nikivuja damu... Unajua nini kilitokea? Kutokana na huruma waliyokuwa nayo wanachi juu ya yule mama aliyeibiwa walikuwa na uchu wa kumjua huyo kibaka aliyemwibia ili wamfunze adabu, kwahiyo yule mama alikuwa akijaribu kumkumbuka kijana anayemtilia mashaka huku akisikilizwa kwa makini na wenyeji wa pale Ilala sokoni wakiamini wataweza kumfahamu kama yule mama akijieleza vizuri kwakuwa wezi wote wa pale wanafahamika sana, binafsi mimi kama ningeulizwa ni kwanini nimepigwa vile ningesema ni kwasababu ya kufanana na huyo kibaka! Lakini ukweli ni kwamba yule dada ndiyealiyenisababishia na ndiye aliyeniokoa kwenye kipigo kinono cha wananchi wenye hasira kali na kuna wakati nilimuona kijana akiwa na galoni flani akionekana na ghadhabu kubwa isiyo na utani wala subira katika maamuzi akisema..."Jeshiiii.... Oyaah jeshi wese hili hapa arifuu... Letemoto.... Leteni moto wamezidi kutusumbua hawaa... 'ku...nina' zao" akimalizia na kunitukana! Mawazo yakikristo yakanijia nikaamua kujikabidhi mbele za Mungu, nikafumba macho nikaweka mikono yangu kichwani kama mwanamke aliyefiwa na mumewe, "Eeh Mungu uliye hai tazama mwanao ninahukumiwa bila....." kabla sijamalizia nilijikuta kufumbua macho baada ya kipigo kukoma ghafla na kusikia sauti ikiamuru kijeshi,,,"Nimesema mwacheni haraakaa!!!" Kumbe wale akina dada waliposema ni mimi huku wakininyooshea kidole walimaanisha ni mm waliyeniona kwenye tangazo la tiGO na siku hiyo waliponiona live ikawa wanaonyeshana na kitendo kile kikaendana na utambuzi wa kibaka kwenye tukio lile na kama inavyojulikana wananchi wenye hasira kali ukisema neno mwizi huyu hawasubiri kuelekezwa ameiba nn wao ni kutoa huduma ya kipigo tu na ndio hicho kilichonikumba mm, hakuna aliyetaka kuhoji nilivutwa pale mlangoni kama umeme nikapokelewa na mateke, ngumi, vibao na wengine walitamani hata kuning'ata na nakumbuka nilibahatika kugundua milio mitatu iliyolia kwenye mashavu yangu ilikuwa ni milio ya kandambili alizokuwa akinipostia yule mama aliyeibiwa... Sikumbuki ni nani aliyenichukulia ila niligundua kuwa nimeibiwa kila kitu mfukoni mwangu hadi leso ya mafua ambayo nadhani kwa wakati ule ningeitumia kufutia damu.... Kutokana na maswahibu hayo nilitamani nisijulikane tena kama mimi ndiye Ballo kama akina dada wengi wanavyoniita hivi sasa kila ninakokatiza “Hey Ballo ntaweza kupata chakulacha jioni nawewe leo?” hiyo ndio imekuwa salamu yao hivi sasa na huwa wanaachia tabasamu pana wakiwa wanatamka hayo maneno… “Pole sana kaka yangu najua ni mimi ndiye niliyekusababishia yote hayo…” alisema yule dada aliyeniponza nikapigwa huku akinielekeza kuingia kwenye tax na safari ya kuelekea hospitali ianze, sina la kusema kwa wakati huo hata wewe unadhani ungesema nini sasa kama ni umaarufu ndio huo unakuponza unaibiwa kila kitu, hivi hapa sina hata kitambulisho cha mpiga kura, simu yangu sijui mshkaji alipopiga akanikosa alinichukuliaje? Nadhani ataamini nimemzingua kama mastar wengine walivyojaa mizinguo hadi kwenye misiba… “Jesca sasa si itabidi tupitie nyumbani nkachukue hela ili tumpeleke Ballo hospital au wewe ulibeba hela?” aliongea yule dada kushauriana na mwenzie… “lakini Joy kama itawezekana angeoga kwanza na tukamtafutia shati lingine akabadili…” alishauri Jesca na kuahidi kununua… “Hata hiyo surual imechafuka sana itabidi abadili pia…” alishauri yule dada aliyeniponza ambaye nilisikia akiitwa Joy… Tuliendelea na safari ya kuelekea kwao sikupafahamu wala sikutaka kuuliza akili yangu ilikuwa inawaza sanaa ninayofanya na umaarufuulivyotaka kunitoa roho ila sijui kwanini wale watu waliokuwa wananipiga hawakuweza kunitambua kama mimi ni Ballo? Au lile tangazo halijaangaliwa na watu wote nini? Wakati nayatafakari hayo bila majibu niliweza kugundua kuwa yule dada mwenzao ambaye sikumsikia akiongea lolote hata kushauri lolote kumbealikuwa akiniangalia muda wote na alionekana kujadili kitu kwenye mawazo yake ila kila ninapogeuka kumtazama alipokuwa amekaa upande wangu wa kushoto alikuwa anakwepesha macho ili tusikutanishe macho yetu. Kwakuwa nilikuwa na maumivu ya kipigo cha kibaka na majuto ya kuwa Ballo wala sikuweza kugawa akili yangu na kuweza kusoma hisia za yule dada… Tulifika nyumbani wakaniambia nishuke ni nyumba yenye gate jeusi ipo maeneo ya Africana jirani na Marie stoppers inaonekana wamepanga pale na wanaishi wao watatu na msichana wa kazi na kulikuwa na mtoto kama wa miaka 5 sasa sikuweza kujua ni wa nani kati ya hao wadada watatu… Sasa sijui yule binti alishajua kuna tukiolimetokea na kuna mgonjwa ataletwa pale! Yaani ni kama alijiandaa maji ya moto yalikuwa tayari alichofanya tu ni kwenda nnje kuchukua taulo liliokuwa limeanikwa na kunipatia “Twende ukaoge kaka…” alisema yule binti wa kazi huku akinishika mkono na hapo ndio maumivu ni kama yamezidi sasa nlikuwa kila mahali pananiuma, Jesca na Joy walienda kunitafutia nguo dukani alibaki yule dada mwingine ambaye hadi muda huo sijasikia akiongea hata alipofika alikaa kwenye kochi kama mgeni vile… Nikajikokota hadi bafuni na bafu lilikuwa humo ndani sijui kwanini nilikuwa sina hata hofu yaani utadhani nipo kwa Mjomba yangu Mikoroshini vile… Nikaanza kuoga na maumivu natamani kuacha maana hata mkono kufika kichani ni mbinde ili nijipake sabuni, lakininkajitahidi kiume… “Heeeeh!!!” nilijikuta natoa sauti kwa kusema hivyo kwa mshangao baada yakumwona yule dada ambaye hajaongea tangu nimuone amesimama mbele yangu katikati ya bafu… Nilibaki kumshangaa yule dada na yeye alikuwa ananiangalia machoni kwa sekunde kadhaa nisijue la kufanya nikamwona akishusha macho yake taratibu kama aliyekuwa akitaka kuukaguamwili wangu kama una makovu na alionekana kama anahuruma hivi anavyoendelea kushusha macho chini kufuatilia mwili wangu lkn sijui kwanini alianza kutetemeka..."Mmmmmh....mmmmmh!" alivuta pumzi ndeefu huku akinisogelea na alionekana kutaka kunikumbatia! Aalaaah hapo machale yakanicheza kumbe alikuwa na lengo la kunijua zaidi ya pale... "Mamdogo... Mamdogoo... Jamani mamdogo kaka wa watu anaumwa huyo muachejamani... Hivi kwanini usijizuie tu hadi unataka kututia aibu jamani?" hiyo ni sauti ya binti wa kazi alikuwa akiita na kumlalamikia yule dada, hata hivyo hakujibu kitu ni kama sio yeye anayeambiwa hivyo akazidi kunisogelea na miminkizidi kurudi nyuma kwa hofu mara nkafikia ukutani akanibamba na kuanza kunipapasa akianzia kifuani jambo ambalo lilinifanya nijisikie fedhea kugeuzwa mtumwa yaan hakunamakubaliano wala upendo wowote pia nkizingatia mwili mzima nilikuwa naumwa kutokana na kipigo cha wananchi... "Samahani dadangu mimi sitaki kufanya chochote aaaah hebu toka bana!" nilisema hivyo na wakati huo nshakasirika na sikutaka tena hata kuendelea kubaki pale lkn kabla sijafanikiwa kuvaa nguo na kutoka yule binti wa kazi aliingia bafuni na kumvuta yule dada ambaye yeye alikuwa anamwita mamamdogo... "Hebu toka nje huoni aibu kumfata mgeni bafuni?" ilikuwa kama yule dada anamuheshimu yule binti wa kazi maana alipoingia tu mule bafuni aliniachia na kukubali kutoka nje lakin ni kama alitoka kwa hasira na sijui kwanini hadi muda huo alikuwa ajatoa sauti yoyote ile achilia mbali kuongea... Nikavaa boxer yangu na suruali haraka haraka bila kujali mwilini nlikuwa na povu la sabuni nkatoka nkitaka kuondoka kufika sebuleni nilishangaa kumkuta yule dada amelala chini akivuja damu nyingi kama bomba la maji.... Unajua ni kipi kilitokea? Kwakua aliondoka mule bafuni kwa hasira alikuwa anatembea bila uangalifu jambo lililomsababishia kukatwa na kioo kilichomdondokea kutoka kilipokuwa kimewekwa dirishani pale kwenye korido alipokatiza na mahasira yake, eti hadi muda huo sijajua sauti yake nkabaki tu namshangaa nakujiuliza huyu ni bubu au vipi? "Ballo umemfanya nini ma mdogo?" ilikuwa ni sauti ya Joy baada ya kurudi na Jesca kutoka dukani kuninunulia nguo... "jamani ma mdogo jamaaaanikwani imekuwaje tena jaman Ballo umemfanyaje?" alilalamika Jesca huku akimnyanyua pale chini akisaidiana na Joy..."wala sio ballo ni yeye mwenyewe dada ameumia!" alinitetea binti wa kazi akitokea ndani na pamba na kichupa kidogo nadhani ni cha dawa... "kwani ilikuwaje?" aliuliza Joy huku akimwachia ma mdogo wake akae kwenye kochi... "Sikia dada huyu Ballo alipokuwa bafuni ma mdogo alimfata na mimi nkaenda kumtoa sasa eti ndio kachukia akatoka kwa hasira akakigusa hicho kioo hapo kwa bahati mbaya ndio kikamkata!" alitoa maelezo hayo binti wakazi... "Eeh ballo pole mwaya kwa usumbufu msamehe tu ma mdogo wetu ni mgonjwa ana pepo wa ngono huwa inatokea anawakamata hadi machinga wanaotembeza urembo!" alielezea joy wakati huo jesca alikuwa anaendelea kumsafisha lile jeraha... "Huduma zao hapa ni nzuri sana yaani" alisema Jesca wakati tukiwa tunaingia kwenye tax baada ya kuhudumiwa pale Marie stopers... "sasa jesca si itabidi tumpeleke Ballo hadi kwake jaman?" alisema joy na wote tukaongozana hadi sinza mori ninapoishi, nilishuka kwenye tax na kuwapamshtuko baadhi ya majirani walioniona asubuhi nkiwa mzima halafu muda huo wananiona nimebandikwa maplasta kibao... "Pole kaka sijui umefanyaje tena ukaumiaa hivyo?" aliuliza dada bonge mwenye duka jirani kabisa na nyumba ninayoishi... "nimeanguka na pikipiki.." nilijikuta namdanganya japokuwa sikujua kwanini nimedanganya na kuingia ndani kupumzika..."hodii! Hodii! Hoooooddiiiiii..." ilikuwa ni sauti nyororo ya mtoto wa mwenye nyumba ya jirani aliyeja pale eti kunipa pole tu halafu eti amevaa kanga moja tu... "ahsante dadangu" nilimjibu yule dada... "kaka mbona hunifungulii mlango? Au hutaki niingie ndani kwako?" alisema yule dada na kuingia ndani baada ya kumfungulia.... Yule dada alipoingia ndani alianza kuniangalia kwa huruma na huku akionyesha kuhuzunika baada ya kuona vidonda vingi nilivyofungwa na baadhi ya sehemu kuwa na uvimbe... "dada usinishike hapo nayasikia maumivu bado" nilimwambia alipokuwa ananishika shika baadhiya sehemu zenye vidonda... "pole sana jamani sasa unakula nn?" aliuliza swali zuri huku akionyesha sura ya kutaka kutoa msaada jambo lililonifanya nikumbuke kuwa kaka yangu ninayeishi naye pale hakuwepo na sikujua nitakula nn na ni muda gani.... "aaaaah si-sina nanii...sijui kama kuna chochote ngoja ntaenda hotelini kwa hapo nje kula maana sitaweza kupika naumwa sana...." nilijieleza kwakujitambua wazi siku hiyo nilitamani kupata usingizi nilale sana na nikiamka nijikute nimepona... "kwani hakuna vitu huku ndani nikusaidie kupika mwaya?" aliuliza kwa sauti ya kubembeleza wakati huo mkono wake wa kulia ukiwa kwenye bega langu la kushoto sikutaka kujiuliza zaidi ni kwanini alikuja pale na kanga moja tena hiyo ikiwa ni tofauti na siku zote anapokuja kumsalimia kakangu, hata hivyo kuna siku alimwita kaka shemeji lkn kakangu akamwambia asimchurie sasa sijui kuna nini kimempa ujasiri wa kuja pale kwenye room ya wanaume na vazi la kanga moja ambalo ni maarufu sana kwenye ulimwengu wa mahaba..."wala usijali dadangu mm ntaenda tu hotelini..." aaah thubutu yake aligeuka ghafla kama aliyekumbuka kitu akiliacha Tako lake laini lililojaaliwa likitikisika na kuanza kuifuata frege kama mwenyeji vile... "sasaa da.." nilishindwa kumalizia kusema baada ya kuyaona maonyesho yaliyokuwa yanaendelea mbele ya macho yangu yaan kumbe hakuvaa chupi, au alivaa nini zile mnaita aaaah nini hebu nikumbusheni zile nanilii... 'Bikin' nadhani ndio vazi pekee lilokuwepo mwilini mwake likisaidiana na ile kanga... "kumbe mboga unayo hapa naona kuna mchele kwanini usile hapa hapa? Acha nkupikie bana..." aliongea hivyo huku akiinama kuchukua sinia kupetea mchele nadhani hadi muda huo nilikuwa nmesahau kuwa mimi ni mgonjwa si nikanyanyuka eti nkamsaminishe... "aaaaaaah!" nililazimika kukaa kwenye kochi na kiherehere choote kikaniishia... Sorry guyz nimepigiwa simu ntaendelea tena kesho... Kwa ushauri na maoni tupia inbox au my# 255654741434 Niite Erick a.k.a 'Ballo'