Sunday, July 20, 2014

BILIONI 23

Kampuni ya upili kwa ukubwa katika
utengenezaji wa sigara nchini Marekani
imeagizwa kulipa kitita kikubwa cha dola
billioni 23 kwa mke wa mwathiriwa mmoja wa
sigara aliyefariki kutokana na saratani ya
mapafu.
Kwa mujibu wa shirika la habari la BBC, Mjane
huyo Cynthia Robinson alichukua hatua dhidi
ya kampuni ya sigara ya R.J Reynolds baada
ya kifo cha mumewe aliyekuwa na miaka 36.
Kampuni hiyo imeyataja malipo hayo kama
yasio na haki na kusema kuwa itakata rufaa.
Wakili wa bi Robinson amesema kuwa kampuni
hiyo ya sigara iliuza sigara hizo bila kutoa
tahadhari yoyote kuhusu tishio la uvutaji wake.