Friday, July 18, 2014

SIO MOTO

Baada ya kusambaa picha
zinazoonesha hotel ya Sanawari
ikiungua moto, Kamanda wa
Polisi mkoa wa Arusha akanusha
posted 3 hours ago by admin
Kumekuwa na taarifa na picha zinazoeleza kuwa
hotel ya kifahari ya Sanawari iliyoko karibu na
mataa ya Sanawari jijini Arusha inateketea kwa
moto.
Hata hivyo, kamanda wa polisi wa mkoa Arusha,
Liberatus Sabas ameiambia 100.5 Times Fm kuwa
habari hizo sio za kweli kwani hata yeye yuko
karibu na eneo hilo kiasi cha kuweza kuiona hotel
hiyo kwa mbali.
“Mimi siko kwenye hotel ya Sanawari lakini niko
karibu na hotel hiyo na kama kungekuwa na moto
nigeona.” Amesema Kamanda Sabas.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja kilichoko jijini
Arusha, kikosi cha zima moto kimefika katika hotel
hiyo na kukuta mambo yako shwari na hakuna dalili
zozote za moto katika jengo hilo.