
Mwanamuziki maarufu na mwenye umri mkubwa kuliko nchini Tanzania, Bi 
Kidude, amefariki dunia leo hii akiwa Zanzibar, alikuwa anaumwa na 
alipowahishwa hospitali haikuwa rizki tena.
 Taarifa ya kifo chake ilitolewa na mpwa wake Baraka Abdulrahman Alisema Bi Kidude alifariki hospitalini kutokana
 na maradhi ya kisukari na uvimbe kwenye Kongosho.
Bi Kidude amekuwa katika fani ya muziki wa taarab ya kiasili pamoja na ngoma za unyago kwa zaidi ya robo tatu ya umri wake.
Katika miaka ya karibuni afya yake imekuwa 
ikizorota kiasi cha serikali ya Zanzibar kumzuia kupanda majukwaani 
kuburudisha japokuwa alionekana katika tamasha la Sauti za Busara mwezi 
Februari mwaka huu.
Mipango ya mazishi ya nguli huyu inafanywa nyumbani kwake  Zanzibar.


Bi kidude akiwa na Prof Jay

 
