Sunday, April 14, 2013

MIMI NI BALLO

Ilikuwa siku ya ijumaa nlipokea sms,"hi, hw ru boy?
Hv ni wewe unayeonekana kwenye tangazola tiGO?
Plz nijibu... Lucy"nkitafakari ni new # lkn hakuna
haja ya kumficha, nkachukua maamuzi ya
kibinadamu nkamjibu,"hi back, i'm fne, ni mm ndio
dadangu..."ilinichukua muda wa 3hrs nkapata tena txt"Je, unaishi dar sehemu gani?"kwakuwa
sikuisave ile namba ya Lucy nkajikuta
najibu"samahan nani mwenzangu? Napenda
kukufahamu kabla sijakuambia nilipo.."akapiga
akalalamika..."jaman Erick ujasave my #? Sawa bana
ndo zenu mkishakuwa mastaa!"nkamfafanulia,"mbona hii ni mara yangu ya
kwanza kuongea na ww? Dadangu nikumbushe
samahani bado cjajua ww ni nani
mwenzangu?"akaongeza pozi..."kwani hakuna
namba iliyokutumia txt leo inafanana na hii?"mmmh
nkavuta kumbukumbu txt kama 21 nmezipokea kwa siku hiyo na new # ni kama 6 sasa ni ipi kati ya
hizo? Ikabidi nmsihi anikumbushe"hiyo txt ilikuwa
imeandikwaje best?"akapata maudhi na kunichana
live..."aaah wapi unajidai ukumbuki Erick yaan
kitangazo kimoja tu unaleta pozi hivyo kakangu
ungekuwa Kanumba je? Yaan huikumbuki hii namba ww?"hapo nilianza kuingiwa na fikra za
taarabu..."Samahan dadangu, unaniruhusu kukata
simu, au unahita kupata kifurushi cha dharau kutoka
kwangu?"hivyo ndivyo uungwana ulivyoniagiza
kumjibu..."aaaah kwenda huko kwanza tangazo
lenyewe lile aaagh ms*#?!* nn?"akakata simu... Kwakuwa nlikuwa namwandikia script mwana
akagonge video ya ngoma yake, alipatwa mshangao
sana kuniona nikiiangalia ile simu na sura yangu
ikionyesha kuchukizwa na maongezi yaliyokatishwa
muda huo..."Ballo vipi tena kuna msiba nn?"aliniuliza
mwanangu anaitwa Chriss huwa ananiita Ballo kama a.k.a yangu lkn jina langu siku zote ni Erick..."aaah
basi tu kuna dada kaniudhi tu halafu hata
simfahamu, na hatak hata kujitambulisha! Aaagh
basi tena ndio kashantukana tuendelee na kazi,
nikayeyushia na kurudi mzigoni... Siku ile ilipita na
maisha yakaenda kama kawaida wala sikuwaza kumpigia yule dada, hata hakuntxt siku inayofata
kuna kimeo nilipata maeneo ya Victoria nkatimba na
wanangu kama vile bongo ilivyo wakachagua cast
zao walizopanga sisi wengine ikawa kama
tunasindikiza tu, majina yetu na picha zikakusanya
sisi tukawa tupo nje tunasubiri na kubadilishana mawazo akaja mshkaji akapenda kujua..."Ballo
kwann unaonekana tofauti sana na lile tangazo? Au
yule ni kakayako nn? Mbona kuleni kama umezeeka
zaidi ya ulivyo?"wanangu wakanijibia kuwa lile
tangazo lilikuwa na lengo la kupata sura za
kitanzania so ilibidi editor anitengeze vile kupata kile wanachohitaji.. . Heeh eti aliondoka na baada ya dk4
akarudi na warembo kama wanne nao walikuja
kunipongeza kwa kula shavu tukafahamiana kumbe
ni models, storry hapa pale hadi muda wa kuitwa
majina wakachaguliwa waliochaguliwa sisi tukasepa
yule mshkaji akaniomba # nikampa ila sijui kwann nlisahau kuchukua ya kwake! Iyo ilikuwa jumamosi
ilipofika j2 nlitoka sinza mori nakoishi nkapanda gari
za gongolamboto niende ilala yule mwana alinipigia
jana yake usiku na kujitambulisha yeye ni Salimu
tuliyeonana kule victoria ananialika kwenye party ya
birthday ya moja ya wale warembo walionisalimia na inafanyika suncirt beach so niwahi tuondoke nae...
Dar foleni kama kawa lkn ilizidi sana maeneo ya ilala
sokoni kuna wakati hadi unatamani kushuka
uchukue bodaboda ila nkavumilia tu,"Nkimuona
ntamjua tu.. Ilikuwa ndio napeleka kwenye M-Pesa
jamani mimi jamaaani...!!!" ilikuwa ni sauti ya mwanamama akilalamika kwa nnje ameibiwa huku
watu wakikusanyika kujua kilichojiri, kwakuwa
kulikuwa na foleni na mm nlikuwa nimesimama kwa
mlangoni mbele ya konda basi nliweza kushuhudia
vizuri jinsi yule mama alivyokuwa akilia na
kumuonea huruma..."Si huyu hapo jamani ndio yeyee...!"ilikuwa ni sauti ya dada mmoja alikuwa
pembeni kidogo na wenzie wawili akininyooshea
mm kidole... Watu wote waligeuka na kuniangalia na
mm nkibaki kumshangaa yule dada aliyeonekana
kunitambua..."Eeh ndio yeye! Onaa eti
anashangaa!!!"Baada ya sekunde10 nlikuwa katikati ya mgambo na shati langu likiwa limechanika na
puani nikivuja damu... Unajua nini kilitokea?
Kutokana na huruma waliyokuwa nayo wanachi juu
ya yule mama aliyeibiwa walikuwa na uchu wa
kumjua huyo kibaka aliyemwibia ili wamfunze
adabu, kwahiyo yule mama alikuwa akijaribu kumkumbuka kijana anayemtilia mashaka huku
akisikilizwa kwa makini na wenyeji wa pale Ilala
sokoni wakiamini wataweza kumfahamu kama yule
mama akijieleza vizuri kwakuwa wezi wote wa pale
wanafahamika sana, binafsi mimi kama ningeulizwa
ni kwanini nimepigwa vile ningesema ni kwasababu ya kufanana na huyo kibaka! Lakini ukweli ni
kwamba yule dada ndiyealiyenisababishia na ndiye
aliyeniokoa kwenye kipigo kinono cha wananchi
wenye hasira kali na kuna wakati nilimuona kijana
akiwa na galoni flani akionekana na ghadhabu
kubwa isiyo na utani wala subira katika maamuzi akisema..."Jeshiiii.... Oyaah jeshi wese hili hapa
arifuu... Letemoto.... Leteni moto wamezidi
kutusumbua hawaa... 'ku...nina' zao" akimalizia na
kunitukana! Mawazo yakikristo yakanijia nikaamua
kujikabidhi mbele za Mungu, nikafumba macho
nikaweka mikono yangu kichwani kama mwanamke aliyefiwa na mumewe, "Eeh Mungu uliye
hai tazama mwanao ninahukumiwa bila....." kabla
sijamalizia nilijikuta kufumbua macho baada ya
kipigo kukoma ghafla na kusikia sauti ikiamuru
kijeshi,,,"Nimesema mwacheni haraakaa!!!"
Kumbe wale akina dada waliposema ni mimi huku wakininyooshea kidole walimaanisha ni mm
waliyeniona kwenye tangazo la tiGO na siku hiyo
waliponiona live ikawa wanaonyeshana na kitendo
kile kikaendana na utambuzi wa kibaka kwenye
tukio lile na kama inavyojulikana wananchi wenye
hasira kali ukisema neno mwizi huyu hawasubiri kuelekezwa ameiba nn wao ni kutoa huduma ya
kipigo tu na ndio hicho kilichonikumba mm, hakuna
aliyetaka kuhoji nilivutwa pale mlangoni kama
umeme nikapokelewa na mateke, ngumi, vibao na
wengine walitamani hata kuning'ata na nakumbuka
nilibahatika kugundua milio mitatu iliyolia kwenye mashavu yangu ilikuwa ni milio ya kandambili
alizokuwa akinipostia yule mama aliyeibiwa...
Sikumbuki ni nani aliyenichukulia ila niligundua
kuwa nimeibiwa kila kitu mfukoni mwangu hadi leso
ya mafua ambayo nadhani kwa wakati ule
ningeitumia kufutia damu.... Kutokana na maswahibu hayo nilitamani nisijulikane tena kama
mimi ndiye Ballo kama akina dada wengi
wanavyoniita hivi sasa kila ninakokatiza “Hey Ballo
ntaweza kupata chakulacha jioni nawewe leo?” hiyo
ndio imekuwa salamu yao hivi sasa na huwa
wanaachia tabasamu pana wakiwa wanatamka hayo maneno… “Pole sana kaka yangu najua ni mimi
ndiye niliyekusababishia yote hayo…” alisema yule
dada aliyeniponza nikapigwa huku akinielekeza
kuingia kwenye tax na safari ya kuelekea hospitali
ianze, sina la kusema kwa wakati huo hata wewe
unadhani ungesema nini sasa kama ni umaarufu ndio huo unakuponza unaibiwa kila kitu, hivi hapa
sina hata kitambulisho cha mpiga kura, simu yangu
sijui mshkaji alipopiga akanikosa alinichukuliaje?
Nadhani ataamini nimemzingua kama mastar
wengine walivyojaa mizinguo hadi kwenye misiba…
“Jesca sasa si itabidi tupitie nyumbani nkachukue hela ili tumpeleke Ballo hospital au wewe ulibeba
hela?” aliongea yule dada kushauriana na mwenzie…
“lakini Joy kama itawezekana angeoga kwanza na
tukamtafutia shati lingine akabadili…” alishauri Jesca
na kuahidi kununua… “Hata hiyo surual imechafuka
sana itabidi abadili pia…” alishauri yule dada aliyeniponza ambaye nilisikia akiitwa Joy…
Tuliendelea na safari ya kuelekea kwao
sikupafahamu wala sikutaka kuuliza akili yangu
ilikuwa inawaza sanaa ninayofanya na
umaarufuulivyotaka kunitoa roho ila sijui kwanini
wale watu waliokuwa wananipiga hawakuweza kunitambua kama mimi ni Ballo? Au lile tangazo
halijaangaliwa na watu wote nini? Wakati
nayatafakari hayo bila majibu niliweza kugundua
kuwa yule dada mwenzao ambaye sikumsikia
akiongea lolote hata kushauri lolote kumbealikuwa
akiniangalia muda wote na alionekana kujadili kitu kwenye mawazo yake ila kila ninapogeuka
kumtazama alipokuwa amekaa upande wangu wa
kushoto alikuwa anakwepesha macho ili
tusikutanishe macho yetu. Kwakuwa nilikuwa na
maumivu ya kipigo cha kibaka na majuto ya kuwa
Ballo wala sikuweza kugawa akili yangu na kuweza kusoma hisia za yule dada… Tulifika nyumbani
wakaniambia nishuke ni nyumba yenye gate jeusi
ipo maeneo ya Africana jirani na Marie stoppers
inaonekana wamepanga pale na wanaishi wao
watatu na msichana wa kazi na kulikuwa na mtoto
kama wa miaka 5 sasa sikuweza kujua ni wa nani kati ya hao wadada watatu… Sasa sijui yule binti
alishajua kuna tukiolimetokea na kuna mgonjwa
ataletwa pale! Yaani ni kama alijiandaa maji ya moto
yalikuwa tayari alichofanya tu ni kwenda nnje
kuchukua taulo liliokuwa limeanikwa na kunipatia
“Twende ukaoge kaka…” alisema yule binti wa kazi huku akinishika mkono na hapo ndio maumivu ni
kama yamezidi sasa nlikuwa kila mahali pananiuma,
Jesca na Joy walienda kunitafutia nguo dukani
alibaki yule dada mwingine ambaye hadi muda huo
sijasikia akiongea hata alipofika alikaa kwenye kochi
kama mgeni vile… Nikajikokota hadi bafuni na bafu lilikuwa humo ndani sijui kwanini nilikuwa sina hata
hofu yaani utadhani nipo kwa Mjomba yangu
Mikoroshini vile… Nikaanza kuoga na maumivu
natamani kuacha maana hata mkono kufika kichani
ni mbinde ili nijipake sabuni, lakininkajitahidi kiume…
“Heeeeh!!!” nilijikuta natoa sauti kwa kusema hivyo kwa mshangao baada yakumwona yule dada
ambaye hajaongea tangu nimuone amesimama
mbele yangu katikati ya bafu… Nilibaki kumshangaa
yule dada na yeye alikuwa ananiangalia machoni
kwa sekunde kadhaa nisijue la kufanya nikamwona
akishusha macho yake taratibu kama aliyekuwa akitaka kuukaguamwili wangu kama una makovu
na alionekana kama anahuruma hivi anavyoendelea
kushusha macho chini kufuatilia mwili wangu lkn
sijui kwanini alianza
kutetemeka..."Mmmmmh....mmmmmh!" alivuta pumzi
ndeefu huku akinisogelea na alionekana kutaka kunikumbatia! Aalaaah hapo machale yakanicheza
kumbe alikuwa na lengo la kunijua zaidi ya pale...
"Mamdogo... Mamdogoo... Jamani mamdogo kaka
wa watu anaumwa huyo muachejamani... Hivi
kwanini usijizuie tu hadi unataka kututia aibu
jamani?" hiyo ni sauti ya binti wa kazi alikuwa akiita na kumlalamikia yule dada, hata hivyo hakujibu kitu
ni kama sio yeye anayeambiwa hivyo akazidi
kunisogelea na miminkizidi kurudi nyuma kwa hofu
mara nkafikia ukutani akanibamba na kuanza
kunipapasa akianzia kifuani jambo ambalo lilinifanya
nijisikie fedhea kugeuzwa mtumwa yaan hakunamakubaliano wala upendo wowote pia
nkizingatia mwili mzima nilikuwa naumwa kutokana
na kipigo cha wananchi... "Samahani dadangu mimi
sitaki kufanya chochote aaaah hebu toka bana!"
nilisema hivyo na wakati huo nshakasirika na
sikutaka tena hata kuendelea kubaki pale lkn kabla sijafanikiwa kuvaa nguo na kutoka yule binti wa kazi
aliingia bafuni na kumvuta yule dada ambaye yeye
alikuwa anamwita mamamdogo... "Hebu toka nje
huoni aibu kumfata mgeni bafuni?" ilikuwa kama
yule dada anamuheshimu yule binti wa kazi maana
alipoingia tu mule bafuni aliniachia na kukubali kutoka nje lakin ni kama alitoka kwa hasira na sijui
kwanini hadi muda huo alikuwa ajatoa sauti yoyote
ile achilia mbali kuongea... Nikavaa boxer yangu na
suruali haraka haraka bila kujali mwilini nlikuwa na
povu la sabuni nkatoka nkitaka kuondoka kufika
sebuleni nilishangaa kumkuta yule dada amelala chini akivuja damu nyingi kama bomba la maji....
Unajua ni kipi kilitokea?
Kwakua aliondoka mule bafuni kwa hasira alikuwa
anatembea bila uangalifu jambo lililomsababishia
kukatwa na kioo kilichomdondokea kutoka
kilipokuwa kimewekwa dirishani pale kwenye korido alipokatiza na mahasira yake, eti hadi muda
huo sijajua sauti yake nkabaki tu namshangaa
nakujiuliza huyu ni bubu au vipi? "Ballo umemfanya
nini ma mdogo?" ilikuwa ni sauti ya Joy baada ya
kurudi na Jesca kutoka dukani kuninunulia nguo...
"jamani ma mdogo jamaaaanikwani imekuwaje tena jaman Ballo umemfanyaje?" alilalamika Jesca huku
akimnyanyua pale chini akisaidiana na Joy..."wala sio
ballo ni yeye mwenyewe dada ameumia!" alinitetea
binti wa kazi akitokea ndani na pamba na kichupa
kidogo nadhani ni cha dawa... "kwani ilikuwaje?"
aliuliza Joy huku akimwachia ma mdogo wake akae kwenye kochi... "Sikia dada huyu Ballo alipokuwa
bafuni ma mdogo alimfata na mimi nkaenda kumtoa
sasa eti ndio kachukia akatoka kwa hasira
akakigusa hicho kioo hapo kwa bahati mbaya ndio
kikamkata!" alitoa maelezo hayo binti wakazi... "Eeh
ballo pole mwaya kwa usumbufu msamehe tu ma mdogo wetu ni mgonjwa ana pepo wa ngono huwa
inatokea anawakamata hadi machinga
wanaotembeza urembo!" alielezea joy wakati huo
jesca alikuwa anaendelea kumsafisha lile jeraha...
"Huduma zao hapa ni nzuri sana yaani" alisema Jesca
wakati tukiwa tunaingia kwenye tax baada ya kuhudumiwa pale Marie stopers... "sasa jesca si
itabidi tumpeleke Ballo hadi kwake jaman?" alisema
joy na wote tukaongozana hadi sinza mori
ninapoishi, nilishuka kwenye tax na
kuwapamshtuko baadhi ya majirani walioniona
asubuhi nkiwa mzima halafu muda huo wananiona nimebandikwa maplasta kibao... "Pole kaka sijui
umefanyaje tena ukaumiaa hivyo?" aliuliza dada
bonge mwenye duka jirani kabisa na nyumba
ninayoishi... "nimeanguka na pikipiki.." nilijikuta
namdanganya japokuwa sikujua kwanini
nimedanganya na kuingia ndani kupumzika..."hodii! Hodii! Hoooooddiiiiii..." ilikuwa ni sauti nyororo ya
mtoto wa mwenye nyumba ya jirani aliyeja pale eti
kunipa pole tu halafu eti amevaa kanga moja tu...
"ahsante dadangu" nilimjibu yule dada... "kaka
mbona hunifungulii mlango? Au hutaki niingie ndani
kwako?" alisema yule dada na kuingia ndani baada ya kumfungulia....
Yule dada alipoingia ndani alianza kuniangalia kwa
huruma na huku akionyesha kuhuzunika baada ya
kuona vidonda vingi nilivyofungwa na baadhi ya
sehemu kuwa na uvimbe... "dada usinishike hapo
nayasikia maumivu bado" nilimwambia alipokuwa ananishika shika baadhiya sehemu zenye vidonda...
"pole sana jamani sasa unakula nn?" aliuliza swali
zuri huku akionyesha sura ya kutaka kutoa msaada
jambo lililonifanya nikumbuke kuwa kaka yangu
ninayeishi naye pale hakuwepo na sikujua nitakula
nn na ni muda gani.... "aaaaah si-sina nanii...sijui kama kuna chochote ngoja ntaenda hotelini kwa
hapo nje kula maana sitaweza kupika naumwa
sana...." nilijieleza kwakujitambua wazi siku hiyo
nilitamani kupata usingizi nilale sana na nikiamka
nijikute nimepona... "kwani hakuna vitu huku ndani
nikusaidie kupika mwaya?" aliuliza kwa sauti ya kubembeleza wakati huo mkono wake wa kulia
ukiwa kwenye bega langu la kushoto sikutaka
kujiuliza zaidi ni kwanini alikuja pale na kanga moja
tena hiyo ikiwa ni tofauti na siku zote anapokuja
kumsalimia kakangu, hata hivyo kuna siku alimwita
kaka shemeji lkn kakangu akamwambia asimchurie sasa sijui kuna nini kimempa ujasiri wa kuja pale
kwenye room ya wanaume na vazi la kanga moja
ambalo ni maarufu sana kwenye ulimwengu wa
mahaba..."wala usijali dadangu mm ntaenda tu
hotelini..." aaah thubutu yake aligeuka ghafla kama
aliyekumbuka kitu akiliacha Tako lake laini lililojaaliwa likitikisika na kuanza kuifuata frege kama
mwenyeji vile... "sasaa da.." nilishindwa kumalizia
kusema baada ya kuyaona maonyesho yaliyokuwa
yanaendelea mbele ya macho yangu yaan kumbe
hakuvaa chupi, au alivaa nini zile mnaita aaaah nini
hebu nikumbusheni zile nanilii... 'Bikin' nadhani ndio vazi pekee lilokuwepo mwilini mwake likisaidiana na
ile kanga... "kumbe mboga unayo hapa naona kuna
mchele kwanini usile hapa hapa? Acha nkupikie
bana..." aliongea hivyo huku akiinama kuchukua
sinia kupetea mchele nadhani hadi muda huo
nilikuwa nmesahau kuwa mimi ni mgonjwa si nikanyanyuka eti nkamsaminishe... "aaaaaaah!"
nililazimika kukaa kwenye kochi na kiherehere
choote kikaniishia... Sorry guyz nimepigiwa simu ntaendelea tena kesho...
Kwa ushauri na maoni tupia inbox au my#
255654741434 Niite Erick a.k.a 'Ballo'