`WICCA: Dhehebu la wapagani wanaodai wamezaliwa upya!`
"Mwanzilishi wake ni Mmarekani aitwaye Terry aliyeasi toka Kanisa la Wanazarini"
MJI wa Jonesboro upo katika jimbo la Arkansas huko Marekani. Hapo ndipo yalipo makao makuu ya dhehebu jipya lililoanzishwa la Wicca.Dhehebu
hili la kipagani limeanzishwa na Mmarekani aitwaye Terry mwenye umri wa
miaka 38 akiwa ni mkazi aliyezaliwa na kukulia katika mji huo wa
Jonesboro.
Imani ya kipagani ya "Wicca" inaaimini juu ya mambo
ya asili ikiwa ni pamoja na uganga wa jadi, uchawi, ramli na nguvu za
kimizimu zenye kutenda miujiza.
Hata hivyo jambo la kushangaza ni kuwa "Wicca"ambao
pia hujiita "Born Again Pagans" yaani "wapagani waliozaliwa mara ya
pili"wanadai kuwa wao ni Wakristo sawa na wengine isipokuwa wanaamini tu
juu ya vitu vya asili.
Terry mwenyewe kabla ya kuasi mwaka 1993 na kuanzisha
dhehebu hili la kipagani alikuwa ni muumini hodari wa dhehebu la
kikristo linalojulikana kama "Nazarene Church"
Terry anadai kuwa aliamua kuachana na dhehebu la
"Nazarene"na kuanzisha dini hii ya "Wapagani Waliozaliwa Upya"baada ya
kupata maono ya miujiza kwa miaka 5 mfululizo.
Mji wa Jonesboro jimboni Arkansas Marekani umekuwa ni
chimbuko la madhehebu mapya ya ajabu ajabu yapatayo 75. Kufuatia hali
hiyo ya dini mpya kuzuka katika mji huo kila kukicha watu wameamua
kuubatiza mji huo kwa jina la "Fort God" wakimaanisha ng’ome ya Mungu.
Muumini wa dhehebu hili la kipagani la ‘Wicca"
linaloongozwa na Terry anapaswa kuwa na vifaa mbalimbali vya kichawi na
kimizimu vinavyotumiwa na dhehebu hili wakati wa ibada.Vifaa hivyo
vimekuwa ni pamoja na mifupa, vibuyu,rangi,chupa, vitabu maalum,ngoma,
mishumaa, ubani, udi na uvumba.
Ili kuwarahisishia waumini wake upatikanaji wa vifaa hivyo, Terry amefungua duka kubwa la kuviuza jijini Jonesboro.
Lakini la kushangaza ni kuwa hivi karibuni duka hilo
liliponea chupuchupu kufungwa baada ya mwenye nyumba kumjia juu Terry
akimdai kodi.
Steven Griffin, anayemiliki nyumba ambamo Terry
amefungua duka hilo alifoka kuwa "mimi siogopi miungu yako na ikifika
kesho hujanilipa kodi yangu nitatupa bidhaa zako na kufunga nyumba
yangu"
Kauli hiyo ya Griffin iliwapelekea Wamarekani
kujihoji ikiwa kweli mizimu ya dhehebu hilo la wapagani waliozaliwa upya
inayo nguvu kama kiongozi wao Terry anavyodai.
Terry, yeye kwa upande wake alidai kuwa Grriffin
amehongwa na Kanisa la Nazarene alikokuwa akisali hapo awali kabla ya
kuasi kusudi apate kutibua ustawi wa dhehebu la Wicca katika jiji la
Jonesboro.
Lakini viongozi wa madhehebu kadhaa ya Kikristo huko
Marekani wamelipinga dhehebu la "Wicca"vikali na kuliita kuwa la
kishetani. Mmoja wa viongozi hao ni Mch. Gary Taylor wa Kanisa la
United Christian ambaye anasema "Those kinds of things do not belong in a Christian community. I just don’t believe this is a religion" akimaanisha "Vitu vya aina hiyo havipo katika Ukristo. Kwa kifupi mimi siamini kama hii ni dini"
Dhehebu la Wicca kwa mujibu wa jarida la ‘Times"
limepata kuhusishwa na mauaji ya kikatili ya wavulana 3 yaliyotokea huko
West Memphis jimboni Arkansas. Wavulana hao maiti zao ziliokotwa sehemu
zao za siri zikiwe zimenyofolewa.
Katika maandamano yaliyofanywa hivi karibuni na
wafuasi wa "Wicca" wapatao 75 wakipinga 'kukashifiwa' umati wa wakazi wa
Jonesboro wapatao 2000 waliwazomea wakipiga makelele ya;"You’ll burn in hell!’ "Mtaunguzwa Jehanamu"
Maandamano hayo ya wapagani waliozaliwa upya hatimaye yalidhibitiwa na polisi wa Marekani wapatao 80
Profesa Robi Anderson, ni profesa wa historia katika
Chuo Kikuu cha Arkansas State Univerisity, kilichoko jijini Jonesboro.
Yeye anayo haya ya kusema kuhusu dhehebu hili;"People believe that if its not Christianity its Satanic" yaani
"Watu wanaamini kuwa kama siyo Ukristo basi ni Ushetani bila ya shaka"
Kwa mujibu wa gazeti la Christian Monitor Science
linalochapishwa nchini Marekani, dhehebu la "Wicca" sasa linasambaa kwa
kasi na limeanza kujipenyeza Afrika Magharibi na Mashariki ambapo Kenya
ni moja ya nchi zilizotajwa kuwa nalo, na hakuna ajuaye huenda wapo
Tanzania pia.