Kabla wagonjwa waligongwa kwa nguvu kichwani ili wazirai kabla ya kufanyiwa operesheni
HAPO zamani
kabla dawa ya kutuliza maumivu wakati wa kumfanyia mgonjwa upasuaji
haijavumbuliwa wagonjwa walihisi maumivu makali kwani walifanyiwa huduma
hiyo pasipo kuchomwa dawa yoyote; wakilia na kupiga mayowe yaliyojaza
chumba kizima cha upasuaji michirizi ya damu iliwarukia madaktari
waliotoa huduma hiyo na hata kusambaa chumbani kutokana na kujirusha
rusha kwa mgonjwa.
Kulingana na kitabu cha historia kiitwacho "Who did
it first" kilichoandikwa na Prof. G. C. Thornley mwenye shahada ya juu
ya Phd. katika historia vijana wenye nguvu walihitimiza juu ya meza
anapofanyiwa upasuaji.
Cha kushangaza na kuogofya zaidi ni kuwa wagonjwa
walioneshwa kuwa waoga na wasumbufu waligongwa na kitu sehemu maalum
kichwani ili wazirai halafu daktari akawafanyia upasuaji kwa haraka
kabla hawajazinduka pindi walipozinduka kabla ya operesheni haijaisha
walijikuta wako kwenye maumivu makali kiasi cha kuwapelekea kulaani ni
kwa nini walizaliwa duniani wawe hai kuhisi maumivu hayo.
Profesa Thornley anasema kuwa watu wa kwanza kugundua dawa ya kutuliza maumivu wakati wa upasuaji walikuwa ni Wachina .
Dawa hizi za kienyeji zilizodhaifu na zisingeliweza
kumtulizia mgonjwa maumivu inavyotakiwa pia zilikuwa na madhara yake
kwani kama ulitumia nyingi kwa makusudi ili mgonjwa asiumie, zilimzidi
nguvu na kumuua pia kama ulituma kidogo hazikufaa kitu na mgonjwa
alihisi maumvu maradufu.
Baada ya mwaka 1970 Joseph Priestley, kwa mara ya
kwanza alivumbua gesi iliyofikiriwa ingelifaa kutumiwa kwa kazi hii.
Gesi hiyo ndiyo ile ambayo leo yaitwa "Laughing gas" kwa zaidi ya miaka
30 toka Priestley aivumbue hakuna mtu aliyeitilia maanani.
Lakini mwaka 1800, Sir. Humphry Davy aliweza
kuthibitisha faida zake hata akaipa jina ambalo imedumu kuitwa hivyo
hata leo "Nitrous Oxide" Sir. Humpherey alipendekeza kuwa gesi hiyo
ingefaa kutuliza maumivu wakati wa upasuaji lakini miaka ikazidi
kuyoyoma huku kukiwa hakuna daktari aliyechukua hatua za kuitumia kwenye
upasuaji.
Lakini kunako mwaka 1824, Daktari mmoja aitwaye
Hichman alisoma kwa makini vitabu vya Sir. Humphery ndipo akaamua
kuijaribisha gesi hii kwa mbwa na wanyama wengineo.
Akaibuka na matokeo mazuri sana lakini Hichman akafa angali kijana katika umri wa miaka 29 tu.
Baada ya hapo gesi hii iliyojulikana kama "Laughing
gas" au "Gesi ya vicheko" ilianza kutumiwa kwenye kumbi za dansi huko
Marekani; waliipuliza wakati wa kucheza muziki, ikawalewesha na
kuwapelekea kucheka hovyo na kufurahi sana.
Lakini mtu mmoja aitwaye Horace Wells alienda katika
ukumbi mmoja wapo wa dansi akawachunguza vijana wale kwa makini na
kugundua kuwa walipokuwa wakicheka walikuwa pia hawahisi maumivu hata
wakijigonga kwenye vitu.
Horace Wells aliamua kuifanyia gesi hiyo majaribio
mwilini mwake. Yeye mwenyewe alijipulizia gesi hiyo ikamlewesha kisha
akamwambia rafiki yake amng’oe jino lake moja na huyo rafikie
akafanikiwa kumfanyia Horace huduma hiyo pasipo kuhisi maumivu yoyote.
Horace Wells alianza kujivunia ugunduzi wake kote
katika Marekani lakini alisahau kitu kimoja kuwa hakuwa na hakika ni
kipimo kiasi gani kilihitajika cha gesi ili mtu asisikie maumivu
anapong’olewa jino.
Alienda katika shule moja na kauwafanyia wanafunzi
majaribio ya kuwang’oa meno kwa kutumia gesi hiyo lakini kila mwanafunzi
aliyemfanyia jaribio hilo alilalamika kuwa anahisi maumivu makali .
Well aliamua kurudia jaribio lake kwa mwanafunzi mmoja akidhani kuwa safari ya kwanza labda aliwapa dozi ndogo ya gesi.
Lakini safari hii alijisahau akampulizia gesi kupita kiasi mwanafunzi huyo akafa palepale wakati akimfanyia majaribio.
Tukio hilo lilimchanganya akili Bw. Horace Well aliyependa kusifiwa.
Hivyo Well akapagawa na akachukua hatua ya kujiua mwenyewe kufuatia jaribio lake kushindwa.
Baada ya kifo cha Well daktari mmoja bingwa wa
majaribio ya kisayansi aliyeitwa J.Y. Simpson aliona upo umuhimu wa
kuiendeleza dawa ya gesi, iliyowashinda wataalam wengi kukamilisha na ni
yeye ndiye aliyekuja kufanikiwa kutengeneza dawa ya kwanza ya
kupunguza maumivu wakati wa upasuaji.
Simposon alizaliwa katika familia ya wazazi maskini
sana lakini mama yake mzazi alitaka kuona mwanaye anakuwa na maisha
mazuri siku za usoni.
Walimpeleka katika Chuo Kikuu cha Edinbugh ambako
aliweza kusomea shahada zote za juu kabla ya kuamua kujitosa kwenye fani
ya Udaktari.
Wakati huo daktari mmoja aitwaye Robert Liston
alifanikiwa kumfanyia mgonjwa operesheni ya kukata mguu jijini London
kwa kutumia dawa yake iitwayo "Either" Dk Liston alitumia dakika 26
kumkata kabisa mgonjwa huyo mguu naye hakuhisi maumivu hata kidogo.
Simpson alisikia habari za operesheni hiyo hivyo
akafunga safari kutoka Edinburgh mpaka London kwenda kuchukua "Either’
aje aifanyie majaribio yeye mwenyewe alifanikiwa kuipata na akarejea
nayo jijini Edinburgh ambako yeye na marafiki zake wawili; Duncan na
Keih walitumia kwa kuifanyia majaribio gesi hiyo.
Mwanzoni Simpson alitaka kuutumia mwili wake yeye
mwenyewe kujaribu gesi hiyo lakini, rafiki zake wakamshauri aijaribishie
kwa wanyama kwanza. Hivyo alimjaribishia mbwa naye akazidiwa na kufa.
Baada ya kuifanyia utafiti kwa karibu mwaka mzima
Simposon na marafiki zake wawili walijaribisha dawa ya Simposon
aliyoiita "Chloroform"na ikamlewesha Simpson mwenyewe kiasi kwamba
akajikuta amedondoka uvunguni mwa meza.
Halafu Simposon akarudiwa na fahamu akamuona mwenzake
Dk. Duncan akiwa uvunguni mwa kiti akiwa hoi amepoteza fahamu na kuacha
mdomo wazi baada ya kuzidiwa na "Chloroform".
Dk. Keith naye pia alikuwa akijikokota baada ya kurudiwa na fahamu.
Hapo ndipo Simpson akajikuta amegundua dawa ya
kutuliza maumivu wakati wa upasuaji dawa hii ya "Chloroform"aliyoigundua
Simpson ndiyo inayomudu kutumika mahospitalini wakati wa upasuaji hata
leo. Haikuwa lelemama hivyo kufikia uvumbuzi huo.