PROF JAY: LAWAMA ZANGU KUHUSU MZIKI UNAPOELEKEA NAZIPELEKA KWA WASANII MASHABIKI MEDIA NA SERIKALI YENYEWE
aah kusema ukweli
kitu kikubwa kinachotokea ni kwamba, imefika kipindi sasa imebidi wasanii wa
Tanzania inabidi tuamke tuone wapi tunataka tuelekee na pia tuanza kutafakari
ni wapi mziki wetu tunataka uelekee, kwasababu tumefanya mziki huu kwa
mafanikio, tumetoka mbali kwenye sehem za hatari sana na sasa tuna advantage ya
kwamba kiswahili kiswahili kinaenda kama lugha ya kimataifa tumepata mashabiki
nje ya tanzania.....".
ndio maana leo kwenye
account yangu ya twitter nikasema, inafika kipindi sasa tuangalie, kwasababu
kila mmoja anakua anamtupia lawama mwenzake na vitu vingine kama hivi, ni
kwamba tukae kama wasanii kama watanzania tunaotaka tuangalie mziki huu
tunataka tuupeleke wapi....
kiukweli
inavyoonekana anaeuharibu mziki huu sio mtu mmoja....wasanii kama wasanii
unakuta wanaandika mashairi ambayo hayaeleweki hata kwenyejukwaa
perfomance zao vingine havisaidii kuupeleka mziki wetu mbali hata media
inaonekana kucheza nyimbo zingine ambazo kiulweli kabisa hazisaiidii chochote
kwenye mziki wetu wa Tanzania na katika harakati hizi za kuupeleka
mziki wetu kwenye level, "
"lawama
zangu pia nazipeleka kwa mashabiki, kwasababu wana nyimbo zao ambazo wanapioga
simu wanaomba, kwenye matamasha wanasapoti ya watu wengine lakini kiukweli zile
nyimbo hazisaidii chochote, mashabiki saa zingine wanaomba nyimbo ambazo
hazisaidii chochote na zinakuwa mbovu, "
"lakini kitu
ambacho kikubwa kabisa cha mwisho, ni kwamba serikali ina play part vipi katika
swala hili, ikiwa kama baba wa watanzania wote inabidi itoe kauli,kwasababu
wasanii kila siku kilio chao ni kwamba kazi zao zinaibiwa watu wanakosa ubunifu
ndio maana wanaimba vitu ambavyo viko bubble gum, na vitu ambavyo havieleweki,
serikali kama serikali ingejaribu kuangalia jinsi gani ya kuwasaidia wasanii wa
Tanzania especially katika kazi zao, kwenye vitu kama ringtones, lakini pia
katika sheria jinsi gani msanii anaweza kunufaika na kazi zake anayoifanya,
kwasababu hata sasa hivi hizi stika za TRA haziwezi kusaidia kitu stika
zitakuwepo lakini tatizo sugu tumeliacha, tatizo ni wizi wa kazi za
wasanii......." amesema Prof Jay